15 Aprili 2015 - 13:14
Kerry asisitiza kupata muafaka na Iran

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry siku ya Jumatano amesema kuwa anaamini muafaka wa mpango wa nyuklia wa Iran utafikiwa hata kama wapinzani wa muafaka huo wataongeza vipengele vipya vyakukwamisha mbio za muafaka huo

Shirika la habari AhlulBayt(a.s) ABNA: waziri huyo aliyasema hayo alipokuwa katika mjumuiko wa waandishi wa habari huku akisisitiza kuwa: kwakweli kumaliza mazungumzo ya nyuklia na Iran kwa muda mchache uliobaki nikatika masuala mazito yanayotukabili hivi sasa.
John Kerry akizungumza  alipokuwa mjini Berlin kwaajili ya kushiriki katika kikao cha kikundi cha nchi 7 kinachofanyika leo siku ya Jumatano nchini Ujerumani amesisitiza kuwa: tunaamini tutafikia makubaliano na Iran hasa kutokana na azma mheshimiwa Rais wetu lakuendeleza mazungumzo ya kidiplomasia hata kufikia makubaliano baina ya Iran na nchi zenye nguvu duniani hata kama wapinzani wa muafaka huo wataongeza vipengele vipya vyakukwamisha mbio za muafaka huo.
Miungoni mwa masuala muhimu yatakayo zungumziwa leo katika kikao cha kikundi cha nchi 7 nchini Ujerumani ni suala la Iran na  machafuko yanayotokea  mashariki ya kati ikiwemo nchi za Syria, Iraq, Yemen na Palestina.
Kikao hicho cha mawaziri wa nchi hizo 7 ambazo ni Marekani, Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Japani,  Canada na Italy kinafanyika nchini Ujerumani katika mkoa wa Lubeck kwa muda wa siku mbili Jumatano na Alhamisi.