23 Aprili 2015 - 09:48
 Nigeria yavamia ngome kuu ya Boko Haram

Jeshi la Nigeria limeshambulia ngome ya kuu inayojulikana ya kundi la kigaidi la Boko Haram katika msitu wa Sambisa, huku likisaidiwa na ndege za kivita.

Jeshi la Nigeria limeshambulia ngome ya kuu inayojulikana ya kundi la kigaidi la Boko Haram katika msitu wa Sambisa, huku likisaidiwa na ndege za kivita. Haya ni kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyanzo viwili vya habari katika jeshi hilo. Msitu huo wa Sambisa uko umbali wa kilo meta 100 kutoka kijiji cha Chibok ambako Boko Haram iliwachukua mateka wasichana wa shule zaidi ya 200 mwaka mmoja uliopita. Maafisa wa kijasusi waliamini kuwa wasichana hao wanashikiliwa katika msitu huo, ingawa ndege za Marekani zisizo na rubani zimeshindwa kuwaona. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Afrika Magharibi Mohammed Ibn Chambas amesema mwezi huu kwamba huenda wanamgambo wa Boko Haram wanaojificha katika msitu wa Sambisa wanawatumia baadhi ya wasichana waliowateka kama ngao yao.