Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema leo anataraji kwamba Ugiriki inaweza kufikia haraka makubaliano ya kupatiwa msaada wa uokozi ili isifilisike lakini amesisitiza kwamba serikali ya nchi hiyo lazima ionyeshe nia ya kufanya mageuzi.Akizungumza katika kampeni ya uchaguzi wa jimbo huko Bremen kabla ya uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mwezi ujao Merkel amesema kwa upande wa Ujerumani nchi hiyo iko tayari kutowa msaada itakayombwa lakini lazima mageuzi yatekelezwe.Ametilia mkazo suala la Ugiriki kujitolea kutekeleza mageuzi fulani ikiwa ni pamoja na ubinafsishaji ili iweze kupatiwa mikopo ya kuinusuru isifilisike.