28 Aprili 2015 - 11:16
 Umoja wa Ulaya kurefusha muda wa vikwazo dhidi ya Urusi

Kwa mujibu wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Umoja wa Ulaya utaurefusha muda wa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi kutokana na mgogooro wa nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Umoja  wa Ulaya utaurefusha muda wa vikwazo vilivyowekwa dhidi  ya Urusi kutokana na mgogooro wa nchini Ukraine. Kansela Merkel alifahamisha kwenye kikao cha mashauriano baina ya serikali za Ujerumani na Poland kilichofanyika katika  mji mkuu wa Poland, Warsaw kwamba Umoja wa Ulaya  uliamua mwezi uliopita kwamba kuondolewa vikwazo hivyo kutategemea na kutekelezwa kwa ukamilifu makubaliano  yaliyofikiwa mjini Minsk juu ya mgogoro wa Ukraine.