Shirika la habari AhluBayt (a.s) ABNA: taarifa za kuangamia kwa gaidi huyo zimetangazwa na makamanda wengine wa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq.
Msimamizi wa masuala ya ulinzi katika kikundi cha kigaidi cha Daesh katika mji wa Musol nchini Iraq ameangamia akiwa na wasaidizi na walinzi wake katika kambi yao mjini Musol, kufuatia mashambulizi ya anga yaliofanywa na majeshi ya Iraq katika makazi ya kikundi hicho katika wilaya ya Musol.
Mashambulizi hayo yamefanywa kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya ulinzi na usalama vya Iraq, mafanikio hayo ni kutokana na umakini wa vyombo vya usalama vya Iraq mpaka kufanikiwa kuangamiza makamanda wa ngazi za juu wa kikundi hicho cha kigaidi cha Daesh, kitu amba kimeingiza hofu kubwa katika nyoyo za magaidi hao nchini humo.
Katika miezi ya hivi karibuni kikundi cha kigaidi cha Daesh kimepoteza makamanda wake wa ngazi za juu kufuatia mashambuli ya anga ya ndege za Iraq katika makazi ya kikundi hicho katika maeneo mbalimbali katika wilaya ya Musol nchini Iraq.
Wilaya ya Musol toka miaka miwili iliopita iliingia mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh na kutumika sheria ya kikundi hicho katika miji ya wilaya hiyo.
mwisho wa Habari/290
17 Agosti 2016 - 18:05
Msimbo wa Habari: 772649
Kamanda mmoja wa masuala ya ulinzi na usalam katika kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq ameangamizwa na mashambulizi ya anga yaliofanywa na majeshi ya Iraq katika mji wa Musol