29 Desemba 2016 - 15:10
Hatua ya pili yakuikomboa mashariki ya Musol yaanza

Taasisi ya kupambana na ugaidi nchini Iraq imetangaza kuanza kwa hatua ya pili ya mashambulizi ya kuikomboa mashariki mwa Musol kutoka mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Iraq

Shirika la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: viongozi wanaosimamia mapambano dhidi ya ugaidi katika wizara ya mambo ya ndani ya Iraq imetangaza kuendeleza kwa mashambulizi yake dhidi ya magaidi wa Daesh nchini humo, ambapo wameanza kushambulia maeneo yanayokaliwa na magaidi hao kusini mwa mashariki ya Musol.
Televishen ya Almayadin ikinukuu kutoka kwa taasisi ya kupambana na magaidi nchini Iraq imetangaza kuanza hatua ya pili ya kuikomboa mashariki ya Musol kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.
Katika hali hiyo pia viongozi wa wizara ya mambo ya ndani wametangaza kusonga mbele kwa majeshi ya ulinzi nchi humo, kuelekea katika sehemu zinazokaliwa na magaidi wa Daesh kusini mwa mashariki mwa Musol.
Kiongozi mmoja akielezea mashambulio hayo amesema kuwa majeshi ya Iraq baada ya kuanza mashambulio hayo kwa muda wa dakika kumi na tano wameweza kusonga mmbele kwa umbali wa mita 500 katika sehemu zinaokaliwa na magaidi hao.
Aidha ameongeza kusema kuwa: majeshi ya Iraq yako katika hali ya kukumboa sehemu ya “Al-Intisar” ambapo inadhaniwa kwamba majeshi ya polisi zaidi ya elfu 3 ambayo wiki iliopita walitolewa sehemu mbalimbali kuletwa katika sehemu husika watashiriki katika mashambulio hayo.
Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la “Reuters” kutoka mjini Erbil ni kwamba: mashambulizi ya kuikomboa Musol wameshiriki wanajeshi laki moja kutoka jeshi la Iraq, wakishirikiana na majeshi ya wakurd na majeshi ya kujitolea wananchi nchini humo, ambalo lina idadi kubwa zaidi ya majeshi ya ardhi lilioundwa nchini Iraq toka zama ilipovamiwa Iraq na Marekani mwaka 2003.
Waziri mkuu wa Iraq aliahidi kukombolewa kwa mji wa Musol kutakamilika mpaka mwishoni mwa mwaka 2016 ama wiki hii ametangaza kuwa kuikomboa kwa Musol mikononi mwa kikundi cha kigaidi cha Daesh itafanikiwa baada ya miezi mitatu ijayo.
mwisho/290