Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amemteua seneta wa zamani Dan Coats kuwa mkurugenzi wa Shirika la Ujasusi, akisema mtu huyo anafaa kuongoza juhudi za uangalifu, usio na kikomo wa utawala wake dhidi ya wale wanaonuia kuidhuru Marekani. Uteuzi wake huo umefanywa siku moja baada ya kutolewa ripoti ya vyombo vya ujasusi, iliyoituhumu Urusi kuingilia katika siasa za Marekani na katika mchakato wa nchi hiyo wa utunzi wa sera.
Trump anataka kuimarisha mahusiano na Urusi na mara kwa mara amekuwa akilaani mtazamo wa vyombo vya kijasusi kwamba serikali ya Urusi iliingilia katika uchaguzi kumsaidia kupata ushindi dhidi ya mgombea wa chama cha Democratic, Hilary Clinton. Uteuzi wa Coats ambaye ni mrepublican kutoka jimbo la Indiana, utasubiri ridhaa ya baraza la seneti ndipo achukue rasmi uongozi wa shirika hilo la ujasusi lililoundwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001.
Rais Obama ambaye muda wake unaisha mwezi huu, amekuwa akijitahidi kuhahakisha anaharibu mipango ya rais mpya hasa katika mahusiano ya rais huyo na serikali ya Urusi, pia kuhusiana na sera za Obama kusaidia magaidi nchini Syria ambazo zinapingwa vikali na Trump.
Mwisho wa habari/ 291