30 Januari 2017 - 19:44
 Waislamu 6 wauwawa msikitini Canada

Wasilamu sita wameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa wakati watu wenye silaha waliposhambulia msikiti mjini Quebec jana baada ya swala ya usiku ya Isha'a,

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa:Wasilamu sita wameuwawa na wengine wanane wamejeruhiwa wakati watu wenye silaha waliposhambulia msikiti mjini Quebec jana baada ya swala ya usiku ya Isha'a, ambapo waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau alilita shambulio hilo kuwa ni la kigaidi. Polisi wamesema watuhumiwa wawili wamekamatwa, lakini hawakutoa maelezo zaidi, ama kitu gani kimesababisha kufanya shambulio hilo. Hapo mapema Imamu wa msikiti huo alisema watu watano wameuwawa na watu walioshuhudia walisema hadi watu watatu waliokuwa na silaha walifyatua risasi dhidi ya waumini wa kiislamu karibu 40 waliokuwa katika msikiti huo ndani ya kituo cha utamaduni cha waislamu mjini Quebec. Waziri mkuu Justin Trudeau alisema katika taarifa kwamba anashutumu shambulio hilo la kigaidi dhidi ya Waislamu katika kituo hicho cha ibada. Wakati huo huo rais wa Ufaransa Francois Hollande ameshutumu shambulio hilo akisema ni msimamo wa amani na uwazi wa watu wa Quebec ambao magaidi walitaka kushambulia.

Mwisho wa habari/ 291