Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Taarifa kutoka Azerbaijan zinasema wanajeshi wake kadhaa wameuawa wakati wa mapigano katika eneo linalogombaniwa la Nargono-Karabakh huku Armenia na Azerbaijan wakilaumiana kuhusiana na kuibuka kwa mapigano hayo. Wizara ya ulinzi ya Azerbaijan imesema katika taarifa yake iliyotolewa leo hii kwamba vikosi vyake vimepoteza askari wakati eneo lake liliposhambuliwa na majeshi ya Armenia mapema leo hii. Wizara ya ulinzi ya Nargono-Karabakh kwa upande wake imesema askari wa vikosi vya Armenia hawakupata majeruhi yoyote katika mapigano hayo, lakini wanajeshi wa Azerbaijan walioanzisha mapigano ndio waliouawa. Eneo la Nargono-Karabakh linapatikana Azerbaijan, lakini tangu kumalizika kwa vita vya wanaharakati wanaotaka kujitenga wa Armenia mwaka 1994, limekuwa chini ya vikosi vya kikabila nchini Armenia pamoja na jeshi la Armenia. Machafuko yaliyozuka mnamo mwezi Aprili yalisababisha vifo vya askari 75 kutoka pande zote mbili. Na machafuko haya yamekuja baada ya askari watatu wa Armenia kuuawa katika mapigano na majeshi ya Arzebaijan ya tarehe 29 ya mwezi Disemba
Mwisho wa habari/ 291