9 Juni 2017 - 17:18
Mripuko wa kigaidi watokea katika mji wa Karbala nchini Iraq + picha

Gaidi mmoja amejiripua kwa bomu aliokuwa amevaa kabla ya kukamatwa na majeshi ya nchi hiyo asubuhi ya leo katika paki moja iliopo ndani ya makao makuu ya mji wa Karbala nchini Iraq

Shiriki la Habari AhlulBayt (a.s) ABNA: asubuhi ya ijumaa ya leo kumetokea mripuko wa kigaidi katika mji wa Karbala katika moja ya paki ziliopo katika mji huo.
Vyanzo vya usalama katika mkoa wa Karbala vimesema katika mahojiano na televishin ya Alsumairia kuwa: gaidi mmoja aliokuwa amevaa bomu alijiripua asubuhi ya leo kabla ya kukamatwa majeshi ya nchi hiyo katika moja ya paki ziliopo katika makao makuu ya mji huo.
Chanzo hicho kimeongeza kusema kuwa: mripuko huo umesababsha kujeruhi watu 4, huku akisisitiza kuwa idadi kamili ya maafa yaliosababishwa na mripuko huo bado haijafahamika.
Chanzo hicho ambacho kimetaka jina lake lisitajwe ametangaza kuwa majeshi ya ulinzi yamezingira sehemu iliotokea mripuko huo, kwaajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Mkoa wa Karbla katika kilometa 100 upande wa kusini mwa Baghdad (mji mkuu wa Iraq) ni kati ya sehemu zilikuwa na amani, ambapo baadhi ya mida magaidi hujaribu kufanya matukio sehemu hiyo, ambapo vyombo vya usalama wa nchi  hiyo hufanya ulinzi mkali kwaajili ya kuwabaini magaidi hao, ambapo mpaka sasa magidi kadhaa walishakamatwa.

mwisho/290