Shirikia la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: hayo yamesemwa na Benjamin Netanyahu “waziri mkuu wa utawala haramu wa Israel” kuwa Tel Aviv haiko tayari kuendelea kuona majeshi ya Iran yanaendelea kubaki nchini Syria na kuongeza nguvu nchini humo.
Aidha Netanyahu ameongeza kusema kuwa: Iran ambayo lengo lake ni kuangamiza Israel, hivyo basi Israel haitairuhusu Iran kufanikisha mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia.
Kadhalika amedai kuwa kamwe hatutairuhusu Iran ifikie lengo lake la kuiangamiza Israel, hivyo hatukubali kuyaacha majeshi ya Iran yakiendelea kuwepo nchini Syria.
Inasemekana kuwa vyombo vya habari siku ya Jumamosi imesikika nasauti ya miripuko mizito katika mji mkuu wa Syria, ambapo ndege za kivita za Israel zilikuwa zikiwa zinafanya mashambulizi katika sehemu ya Homeh ya kusini mwa mji mkuu huo.
Kwa upande mwingine, baadhi ya vyombo vya habari vimeeleza kuwa makombora hayo yalipigwa kutoka maeneo ya Palestina yaliotekwa na utawala wa kizayuni wa Israel, huku ikibainishwa kuwa lengo kubwa la utawala wa kizayuni wa Israel ni kuangamiza silaha za majesi ya utawala wa Syria iliopo katika maeneo yalikuwa yameshambuliwa.
mwisho/290
3 Desemba 2017 - 16:28
Msimbo wa Habari: 870760
Waziri mkuu wa serikali ya Kizayu ya Israel amesema: Tel Aviv haitaendelea kuruhu majeshi ya Iran kuendelee kubaki nchini Syria