27 Novemba 2018 - 06:16
 Wanajeshi wa Israel wamuua Mpalestina

Mpalestina mmoja ameuawa na jeshi la Israel, baada ya kuwagonga na gari wanajeshi wa Israel

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Mpalestina mmoja ameuawa na jeshi la Israel, baada ya kuwagonga na gari wanajeshi wa Israel na kuwajeruhi 3 miongoni mwao. Jeshi la Israel limesema mwanajeshi mmoja amepata majeraha ya kadri, na wengine wawili walipata majeraha madogo, baada ya mpalestina huyo kuwagonga wanajeshi hao waliokuwa watatembea kwenye foleni kando ya barabara katika eneo la Ukingo wa Magharibi ambalo ni eneo la wapalestina  linalokaliwa kimabavu na Israel. Mwanajeshi mmoja alimpiga risasi na kumuuwa mpalestina huyo. Wapalestina wengi ambao hawana mafungamano na vikundi vyovyote walianzisha wimbi la kuwashambulia walowezi wa Israel kwa kuwagonga na gari kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2015 hadi mapema 2016, lakini wimbi hilo limetulia hivi sasa. Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio la leo, lakini kundi la Hamas limemsifu aliyelifanya, likisema ni jibu, ''uharifu unaosababishwa na kukaliwa kimabavu.

Ikumbukwe kuwa wapalestina wamedhulumiwa ardhi zao na waisrael na wanapojaribu kupaza sauti zao kupigania haki zao, hupigwa risasi na kuitwa kuwa ni magaidi.

Mwisho wa habari / 291