Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya ulinzi na uslama ya Urusi imetangaza kurejea kwa wanajeshi 100 wa majeshi ya anga ya Urusi yaliokuwa nchini Syria.
Kwa mujibu wa ripoti hii, majeshi ya anga ya Urusi baada ya kutekeleza wadhifa wake nchini Syria sasa yamerudi nchini Urusi, kwa upande mwengine wizara ya ulinzi na usalama ya Urusi katika kauli yake iliochapichwa katika vyombo vya habari vya nchi hiyo imesema wanajeshi hao walidhifa wao ulikuwa ni kuhifadhi na kulinda maeneo muhimu ya majeshi hayo nchini Syria.
Katika kauli hiyo imeelezwa kwamba wanajeshi hao wamerejeshwa na ndege za kijeshi za nchi hiyo ambapo wamepokelewa na makamanda, viongozi na familia zao nchini humo.
mwisho/290