1 Januari 2019 - 13:25
Utawala haramu wa Israel wajitoa katika Unesco

Mwakilishi wa utawala haramu wa Isreal katika umoja wa Mataifa ametangaza rasmi kujitoa katika jumuia ya Unesco jumuia ambayo iko chini ya umoja wa Mataifa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mwakilishi wa utawala haramu wa Israel katika umoja wa Mataifa atangaza rasmi kujitoa katika jumuia ya Unesco iliokuwa chini ya Umoja wa mataifa.
Aidha sababu ya utawala haramu wa Israel kujitoa katika jumuia hiyo ni kili walichodai kuwa jumuia hiyo inaonyesha hali ya kuifanyia uadui serikari haramu ya Israel, na kusisitiza kuwa Israel kuanzia mwaka 2019 imejitoa rasmi katika jumuia hiyo inayojihusisha na masuala ya kielimu na tamaduni duniani.
Kwa upande mwingine muakilishi huyo amedai kuwa Unesco inafanya juhudi ya kufuta fungano la Mayahudi na sehemu takatifu ya Quds, ambapo serikali ya utawala haramu wa Israel haiko pamoja kushiriki katika jumuia ambayo inafanya juhudi ya kuikandamiza serikali hiyo.
Alkadhalika inasemekana kuwa serikali ya Marekani pia mwaka uliopita ilijitoa katika jumuia hiyo kwa sababu hizohizo ziliotolewa na utawala haramu wa Israel.    
mwisho/290