Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Burkina Faso imesema karibu watu 46 wameuwawa katika mapigano ya kikabila nchini humo wiki hii. Serikali hiyo imesema mnamo Disemba 31 mara tu baada ya kuingia giza watu waliokuwa katika pikipiki walikivamia kijiji cha Yirgou ambacho kina idadi kubwa ya watu wa kabila la Mossi na kuwauwa watu saba. Siku iliyofuata raia wa kijiji cha Yirgou waliwauwa watu 39 wa jamii ya Fulani ambayo ni ya wafugaji kama kulipiza kisasi. Mapema wiki hii serikali ilikuwa imeliambia shirika la habari la Reuters kwamba ni watu 13 tu waliokuwa wameuwawa. Kaskazini mwa Burkina Faso nchini Mali, machafuko ya kikabila yanachochewa na uwepio wa wanamgambo wa Kiislamu, kwani jamii za Wafulani zinadaiwa kuwaficha magaidi. Burkina Faso imeshuhudia ongezeko la mashambulizi ya Kiislamu katika miezi michache iliyopita wakati ambapo magaidi wanataka kuongeza ushawishi wao katika eneo lote la Sahel.
Mwisho wa habari / 291