23 Januari 2019 - 18:29
Mahathir Muhammad: Israel haina nafasi nchini Malaysia

Mahathir Muhammad amebainisha kuwa nchini yake inaamini kuwa utawala wa Israel ni utawala muovu ambao unahitajika uhukumiwe, huku akisistiza kuwa Waisrael hawana nafasi yeyote nchini mwake

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: Mahathir bin Muhammad ambaye ni waziri mkuu wa Malaysia ameyasema hayo kwa mara nyingine tena kuwa utawala wa haufuati sheria ya kimataifa, na kila siku anaendeleza kujenga vitongoji katika maeneo ya Wapalestina.
Aidha amebainisha hayo katika mkusanyiko wa waandishi wa habari katika makao makuu ya umoja wa mataifa alipokuwa akijibu swali la mmoja kati ya waandishi wa habari kunako serikali ya Malaysia kuzuia kuingia wanamichezo wa Israel nchini Malaysia.
Serikali ya Malaysia mpaka sasa haina fungamano lolote na utawala haramu wa Israel, katika hali ambayo mashindano ya kuongelea yatafanyika nchini humo, ambapo viongozi wa Malaysia wametangaza kuwa hawataruhusu wananchini wanaotoka katika taifa la Kizayuni “Israel” kushiriki katika mashindano hayo, hata kama wasimamizi wa mashindano hayo wataamua kuamisha mashindano nchini humo.
mwisho/290