Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa imetangaza kuiwekea vikwazo vizito Iran haitasitisha kuzalisha makombora ya ballistiska nchini humo.
Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa akibainisha suala hilo amedai kuwa: kwa hakika tumeanza mazungumzo mazito na Iran kuhusu mpango wa kusitisha kuzalisha makumbora ya Ballistiska, ambapo kama mazungumzo hayo hayataleta mafanikio mazuri, basi bilashaka tutaiwekea vikwazo vizito Iran.
Alkadhalika wiki kadhaa ziliopirta msemaje wa wizara ya mambo ya nje wa Ufaransa aliitaka Iran kusitisha kuzalisha makombora ya masafa marefu haraka iwezekanvyo, kwa madai ya kwamba uzalishaji wa makombora hayo unaenda kinyume na mkataba 2231 wa umoja wa mataifa, hivyo Iran inapaswa kusitisha haraka zaidi kuzalisha makombora hayo ambayo yanauwezo wa kubeba Nyuklia.
mwisho/290
26 Januari 2019 - 18:51
Msimbo wa Habari: 926492
Wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa yatoa vitisho vya kuiwekea vikwazo vizito dhidi ya Iran endapo Iran haitasitisha mpango wale wa kuzalisha makumbora ya Ballistiska