Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais Rouhani amesisitiza kwamba Iran itaendelea kutengeneza makombora ya aina mbali mbali bila ya hofu na katu hailazimiki kumuomba idhini yoyote kutekeleza azma yake hiyo.
Wairan wako kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40 ya mapinduzi ya kiislamu yaliyouangusha utawala wa kibaraka wa Marekani Shah Mohammed Reza Pahlavi. Ujumbe mkubwa uliotolewa na kiongozi wa jamhuri hiyo ya kiislamu umesisitiza kwamba nchi hiyo haitompigia mtu yoyote magoti au kuomba ridhaa ya mtu kuendelea na harakati zake za kujiimarisha kijeshi. Hotuba ya rais Rouhani imetilia mkazo kwamba njama zinazofanywa na adui dhidi ya Iran zitashindwa kwa namna zote. Na kuonya kwamba sasa nchi hiyo ya Jamhuri ya kiislamu ina nguvu kubwa zaidi kuliko wakati ilipopambana na Saddam Hussein wa Iraq katika vita vilivyosababisha maafa makubwa na uharibifu kutoka mwaka 1980 mpaka 1988. Ambapo Saddam Husen alisaidia na mataifa ya kiarabu, Marekani na Ulaya lakini hawakuweza kuiangusha serikali ya kiislamu ambayo ilikuwa bado changa.
Rouhani amesema ulimwengu unapaswa kutambua kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo mkubwa zaidi kuliko zamani. Pia ameipuuza miito ya kijuha kutoka Marekani na Ulaya ya kutaka pafanyike makubalino mapya ya kuuzuia mpango wake wa Nuklia.

''Mwaka huu tunasherehekea miaka 40 ya kinachoangaliwa kama siku ya ushindi katika mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979 ya nchi yetu dhidi ya njama za wahalifu Wamarekani,wazayuni na nchi zilizopitwa na wakati za kanda hii ambazo zinataka kuwaangusha watu wetu kupitia shinikizo na vikwazo. Leo uwepo wa umma mitaani katika sherehe hizi za kumbukumbu kote nchini kunamaanisha kwamba njama za maadui zimeshindwa. Uwepo huu unamaanisha kwamba adui hatofanikiwa katika malengo yake ya uovu''
Rouhani pia ameipuuza miito kutoka Marekani na Ulaya ya kutaka pafanyike makubalino mapya ya kuuzuia mpango wake wa Nuklia.L akini kwa upande mwingine Kamanda wa ngazi ya juu katika jeshi la kimapinduzi la Iran amenukuliwa akisema nchi hiyo itaiangamiza kabisa miji ya Israel ya Haifa na Tel Aviv ikiwa Marekani itaishambilia jamhuri hiyo ya kiislamu. Sambamba na hayo miji mbali mbali ya Iran ilifurika umati wa mamilioni ya watu kuanzia Abadan kusiniMagharibi mwa Iran mpaka Mashad kaskazini mashariki mwa nchi hiyo wakisikika wakipaaza sauti za kuilaani Marekani na Israel na kuunga mkono serikali ya Iran.

Mwisho wa habari/ 291