Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kadinali wa Ujerumani Reinhard Marx amewashutumu maafisa wa kanisa katoliki kwa namna walivyoshughulikia kashfa ya miongo kadhaa ya viongozi wa Katoliki ya Kubaka na kulawiti watoto wadogo.
Kadinali Marx aliyasema hayo alipohutubia kwenye mkutano ulioitishwa na kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Francis kujadili udhalimu waliotendewa watoto. Kadinali huyo wa Ujerumani amesema kubakwa na kulawitiwa kwa watoto na vijana kumetokana pia na kutumiwa vibaya kwa mamlaka ndani ya kanisa. Aliongeza kusema mbele ya Papa Francis kwamba maafisa wa kanisa Katoliki wanakiuka haki za watu waliotendewa uhalifu wa kiongono kwa kuhujumu taratibu za uchunguzi kwa kudhamiria. Kadinali Marx amesema mafaili yaliyoorodhesha vitendo vya kidhalimu ambayo yangewezesha kufanyika uchunguzi na kuwabainisha wale waliohusika hayakuwekwa tayari kimakusudi. Mkutano wa Vatican wa siku tatu unaohudhuriwa na wajumbe 190 kutoka kote ulimwenguni unamalizika hii leo Jumapili, na Papa Francis anatarajiwa kuongoza misa na kisha atatoa hotuba.
Viongozi wa kanisa la katoliki wamekuwa wakiwanajisi watoto wadogo wakike na wakiume, huku kanisa na serikali husika zikifumbia macho uovu huu unaofanywa na viongozi wa dini.



Mwisho wa habari / 291