23 Juni 2019 - 04:28
Pentagon: Marekani haitaki kuingia vitani na Iran

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema kuwa, nchi hiyo haina nia ya kuingia vitani na Iran, lakini kwamba italinda maslahi yake katika eneo.

(ABNA24.com) Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema kuwa, nchi hiyo haina nia ya kuingia vitani na Iran, lakini kwamba italinda maslahi yake katika eneo.

Taarifa iliyotolewa Jumamosi na Pentagon imesema kuwa, Washington ipo tayari kulinda askari na maslahi ya Marekani katika eneo la Asia Magharibi na kwamba askari wa Kimarekani wapo tayari kutoa jibu kwa tukio lolote katika eneo hili. Sambamba na kukariri madai yasiyo na ukweli kwamba eti Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetungua ndege yake ya ujasusi isiyo na rubani katika anga ya kimataifa, imedai kwamba hatua hiyo ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Aidha Wizara hiyo ya Ulinzi ya Marekani sambamba na kuthibitisha kwamba askari wa Kimarekani walijitahidi sana kuchukua mabaki ya ndege hiyo iliyotunguliwa na Iran bila mafanikio, imekiri kwamba kwa sasa  Washington haina taarifa zozote kuhusiana na mabaki ya ndege hiyo.

Asubuhi ya Alkhamisi iliyopita, Ofisi ya Mahusiano ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ilitangaza habari ya kusambaratishwa ndege ya ujasusi ya Kimarekani, baada ya ndege hiyo kukiuka anga na ardhi ya Iran katika eneo la Kouh-e-Mobarak katika mkoa wa Hormozgan, kusini mwa nchi hii. Komandi ya kigaidi ya askari wa Marekani katika eneo la Asia Magharibi (CENTCOM) sambamba na kukiri habari hiyo ilidai kwamba ndege hiyo isiyo na rubani ya Marekani ilikuwa bado haijaingia katika anga ya Iran na kwamba eti ilikuwa katika maji ya kimataifa. Kufuatia hatua hiyo, viongozi wa Iran walimtumia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, ushahidi unaothibitisha kwamba ndege hiyo ya Marakeni iliingia katika anga ya nchi hii na kisha kusambaratishwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).



/129