(ABNA24.com) Jeremy Corbyn kiongozi wa chama cha Leba ambacho ndicho kikubwa zaidi cha upinzani nchini Uingereza, alisema jana baada ya Boris Johnson kuchaguliwa na chama chake cha Conservative kuwa Waziri Mkuu kwamba ushindi wa Johnson haukupatikana kwa himaya na ridhaa ya wananchi.
Boris Johnson jana alimshinda mpinzani wake Jeremy Hunt katika uchaguzi wa ndani ya chama cha Conservative wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Theresa May.
Katika zoezi la uchaguzi wa jana, Boris Johnson alipata kura 92,153 dhidi ya mpinzani wake Jeremy Hunt alipata kura 46,656.
Boris Johnson leo anatarajiwa kuchukua rasmi wadhifa huo na kumrithi mtangulizi wake Theresa May ambaye katika kipindi cha uongozi wake alikabiliwa na misukosuko mingi katika kuiendesha serikali ya nchi hiyo.
Boris Johnson ameahidi kuiondoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya maarufu kama 'brexit' kabla wa mwisho wa mwezi Oktoba, kazi ambayo ilimshinda Theresa May na kumlazimisha kujiuzulu kama Waziri Mkuu.
/129
24 Julai 2019 - 06:46
Msimbo wa Habari: 964030
Kiongozi wa chama cha Leba nchini Uingereza amesema kuwa, kuchaguliwa Boris Johnson kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo hakukufanyika kwa matakwa na uungaji mkono wa wananchi.