(ABNA24.com) Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua dawa sita mpya ikiwa ni katika jitihada za kujitosheleza katika sekta ya uzalishaji dawa nchini.
Kwa mujibu wa taarifa kati ya dawa zilizozinduliwa ni Glorenta ambayo ni mjumuiko wa dawa kadhaa kwa lengo la kupunguza kiwango cha damu na hivyo kudhibiti ugonjwa wa kisukari au diabetes.
Kwa mujibu wa taarifa dawa hii ina uwezo mkubwa ikilinganishwa na dawa za sasa za kutibu kisukari na huweza kupunguza matatizo ya moyo yanayotokana na kisukari. Dawa zingine ambazo zimezinduliwa ni Giomide na Norabex ambazo ni za kutibu magonjwa ya ubongo hasa katika kutibu ugonjwa wa MS.
Dawa nyingine ambazo zimezinduliwa ni Neurapa na Bratiga ambazo ni kati ya dawa muhimu za kutibu saratani na zinachukua mahala pa mbinu ya chemotherapy ambayo huwa na madhara kwa wagonjwa.
Iran imeweza kupata mafanikio hayo katika uga wa utengenezaji dawa ikiwa ni katika jitihada za kujitegemea katika sekta hiyo baada ya Marekani kujiondoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA mwezi Mei 2018 na kuiwekea Iran vikwazo vya dawa.
/129
29 Septemba 2019 - 08:24
Msimbo wa Habari: 979061
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua dawa sita mpya ikiwa ni katika jitihada za kujitosheleza katika sekta ya uzalishaji dawa nchini.