(ABNA24.com) Hayo yamesemwa na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Harakati hiyo ambapo amesisitizia utayarifu wa vikosi vya Hashdush-Sha'abi kwa ajili ya kukabiliana wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh katika mikoa yote ya Iraq.
Amesisitiza kuwa uwepo wa makamanda wa harakati hiyo katika safu ya mbele ya mujahidina, ni suala nyeti na utekelezaji wa juu wa kimajukumu katika kulinda taifa na wananchi wa Iraq.
Naibu Mkuu wa Harakati ya Hashdu-Sha'abi sambamba na kusisitiza utayarifu wa harakati hiyo kwa ajili ya kukabiliana na wanachama wa kundi la Daesh (ISIS) katika maeneo yote ya nchi hiyo, ameongeza kuwa, magaidi hao hawapaswi kuruhusiwa tena kutishia usalama na amani ya Iraq.
Katika taarifa hiyo Abu Mahdi al-Muhandis ameeleza kuwa Jumanne jioni, kikosi namba 44 cha harakati hiyo kilizima shambulizi jipya la genge la Daesh katika eneo la Hatra, kusini mwa jimbo la Mosul.
Aidha Hashdush-Sha'abi imesisitiza kwamba lengo la magaidi hao ni kuibua ghasia katika vijiji na miji midogo ya kusini mwa mkoa wa Nainawa na kaskazini magharibi mwa jimbo la Saladin na kadhalika kukata njia kuu ya mawasiliano ya mkoa huo.
Operesheni ya 'Irada ya Ushindi' ilianza tarehe 7 Julai iliyopita ambapo hatua tatu za operesheni hiyo zimemalizika kwa mafanikkio makubwa.
.........
340