(ABNA24.com) Taarifa iliyotolewa na chuo hicho sambamba na kulaani vikali hatua zilizo kinyume cha sheria na zisizo za kibinaadamu za serikali ya Nigeria za kuendelea kumshikilia mwanazuoni huyo, imeitaka serikali hiyo kumuachilia huru na pia kuchukua hatua ya kumpa matibabu yeye pamoja na mke wake.
Aidha taarifa hiyo imebainisha kwamba ni miaka kadhaa sasa ambapo serikali ya Abuja imekuwa ikitekeleza hatua za kimabavu za kumshikilia Sheikh Ibrahim Zakzaky, kumuwekea mibinyo na pia kuwaua shahidi watu wengi wakiwemo wafuasi wa kiongozi huyo wa harakati ya Kiislamu wakiwemo pia watoto wake.
Aidha Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa cha nchini Iran kimeongeza kwamba, kwa kuzingatia hali mbaya ya kimwili ya shakhsia huyo pamoja na mke wake, inatazamiwa kwamba watu wote walio huru katika pembe za dunia watasimama kutoa radiamali yao ya kupinga dhulma hiyo ya wazi.
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa ni taasisi muhimu ya kielimu na kimataifa inayotoa mafunzo ya kidini kwa lengo la kueneza mafundisho na malezi bora ya Kiislamu kwa wanafunzi wa kigeni.
..........
340