Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sayyid Abdulmalik al Houthi ameongeza kuwa lengo kuu zaidi la mapindzi hayo ni kujikomboa na kuwa huru nchi ya Yemen. Kiongozi huyo wa harakati ya Ansarullah aliyasema hayo jana katika hotuba iliyotolewa kwa mnasaba wa madhimisho ya mapinduzi ya Septemba 21 nchini humo.
Abdulmalik al Houthi ameongeza kuwa, mfumo wa kisiasa uliopita haukuwa na ufahamu kuhusu uwezo wa wananchi wa Yemen na uliamini kwamba wananchi hawawezi kusimama kidete mbele ya uingiliaji wa Marekani na kulinda kujitawala na uhuru wao.
Al Houthi ameashiria pia matatizo yanayowakabili watu wa Yemen na kusema: Ugumu wa maisha unaowasibu Wayemeni ni matokeo ya vita vya pande dhidi ya taifa hilo, kuzingirwa nchi na kuzuia kuingizwa mafuta na mapatano yanayotokana na bidhaa hiyo.
Wananchi wa Yemen tarehe 21 Septemba mwaka 2014 walifanya maandamano ya nchi nzima wakilalamikia utendaji dhaifu wa serikali ya muda ya Abdu Rabbu Mansour Hadi katika kusimamia masuala ya nchi; na harakati ya Ansarullah ilichukua uongozu baada ya kuingia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Sana'a.
342/