24 Januari 2021 - 15:18
Palestina yaishtaki rasmi Imarati Umoja wa Mataifa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyadh al Maliki amewasilisha rasmi mashtaka dhidi ya Imarati kwa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Gazeti la Al Qudsul-Araby limeripoti kuwa, Mamlaka ya Ndani ya Palestina imeishtaki Imarati Umoja wa Mataifa kwa kukiuka sheria za kimataifa zinazohusu marufuku ya bidhaa zinazozalishwa katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vilivyoko kwenye ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Riyadh al Maliki amesisitiza kuwa, mnamo mwaka huu wa 2021, Israel na mashirika yake ya kikoloni na ya kibepari imesaini mikataba ya kibiashara na mashirika kadhaa ya Imarati, makubaliano ambayo yanakiuka "orodha nyeusi" iliyotolewa na ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa inayohusiana na marufuku ya kuamiliana kibiashara na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

342/