Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Kiongozi huyo mwandamizi wa Jihadul Islami amesema kuwa, damu ya mashahidi waliouawa Jumanne iliyopita huko Nablus katu haitapotea bure na kwamba, Wapalestina wataendeleza mapambano na adui Mzayuni katika maeneo yote ya Palestina.
Kadhalika amesema kuwa, operesheni za kijihadi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan katu hazitasita na katika masiku yajayo kutashuhudiwa kusambaratika na kugonga mwamba mahesabu ya adui Mzayuni.
Siku ya Jumanne wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel walitenda jinai nyingine pale walipomiminia risasi gari la Wapalestina katika kitongoji cha al-Makhfieh katika mji wa Nablos katika Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan na kuwauwa shahidi vijana watatu wa Kipalestina.
Hujuma zilizofanywa huko nyuma na utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na jinai ya kinyama ya juzi Jumanne huko Nablos ni mifano ya wazi wa hatua za kigaidi za utawala huo ghasibu.
Wapalestina wamepinga mauaji hayo kwa kulaani jinai hiyo na kusisitiza kwamba, watatoa jibu kwa hujuma hiyo. Wakazi wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan wameamua kugoma na kufunga maduka na vituo vyote vya biashara katike eneo hilo; hatua inayoonyesha kuwa, jinai hiyo iliyotekelezwa na Israel imeibua umoja na mshikamano baina ya Wapalestina.
342/