1 Machi 2022 - 19:04
Syria yalaani propaganda za nchi za Magharibi dhidi ya Russia

Syria imelaani vikali propaganda za nchi za Magharibi, hasa Marekani dhidi ya Russia na kusema zinapotosha ukweli, zinakuza mambo kupita kiasi na zinachochea mgogoro kwa ajili ya kuendeleza satwa yao ya kibeberu duniani.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika taarifa, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema Russia ina kila haki ya kujilinda na kukabiliana na tishio na njama za nchi za Magharibi na hasa Marekani.

Taarifa hiyo aidha imesema, nchi za Magharibi, na hasa Marekani, zimekuwa zikikiuka sheria za kimataifa na zimewaua mamilioni ya watu wasio na hatia katika vita maeneo mbali mbali ya dunia kama vile Vita vya Korea, Vita vya Vietnam na pia vita katika nchi kama vile Afghansitan, Iraq na Syria. Kwa msingi huo nchi za Magharibi hazina ustahiki wa kuzungumza kuhusu sheria za kimataifa.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kusimama kidete kukabiliana na sera za kibeberu za Magharibi na Marekani ambazo ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.

342/