Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hadi sasa jumuiya na mashirika ya kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, yametangaza mara chungu nzima kwamba ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi na Kizayuni ni jambo linalofanyika kinyume cha sheria na kutaka ujenzi huo usimamishwe mara moja, jambo ambalo limepuuzwa na kukejeliwa na utawala haramu wa Israel.
Kikizungumza jana usiku kupitia taarifa, Kituo cha Haki za Binadamu cha Palestina kimesema kwamba kuendelea kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai za kutisha zinazotekelezwa dhidi ya Wapalestina wasio na hatia na utawala ghasibu wa Israel bila shaka kinaushajiisha utawala huo kuendelea kuvunja sharia za kimataifa na hivyo kupata kiburi cha kutekeleza jinai hata kubwa zaidi dhidi ya taifa la Palestina.
Kituo hicho cha Palestina kimeendelea kusema kuwa ujenzi wa vitongoji ni moja ya mbinu muhimu zaidi zinazotumiwa na utawala haramu wa Israel kwa ajili ya kuimarisha satwa na udhibiti wake juu ya Wapalestina.
Kituo hicho cha kutetea haki za binadamu kimeitaka jamii ya kimataifa itumie kipimo kimoja katika kukabiliana na masuala muhimu ya kimataifa na kuuwajibisha utawala haramu wa Israel kuhusu ukiukaji wake mkubwa wa sheria za kimataifa.
Awali Naftali Bennett, Waziri Mkuu wa Israel alikuwa ametangaza kuwa utawala huo wa kibaguzi utaendelea na mipango yake ya kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kinyume kabisa na sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Mwishoni mwa mwaka 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio nambari 3334 likipiga marufuku kila aina ya ujenzi wa utawala wa Israel katika ardhi za Wapalestina unazozikalia kwa mabavu na kusisitiza kuvunjwa na kuondolewa vitongoji vyote vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
342/