9 Aprili 2022 - 14:39
HAMAS yalaani kitendo cha Uturuki na Bahrain cha kuunga mkono utawala wa Kizayuni

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amelaani kitendo cha Uturuki na Bahrain cha kulaani operesheni ya kishujaa ya mwanamapambano mmoja wa Palestina huko Tel Aviv.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Hazim Qasim amelaani kitendo cha ubalozi wa Uturuki katika ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel na pia hatua ya wizara ya mambo ya nje ya Bahrain ya kulaani operesheni ya mwanamuqawama wa Palestina na kusema kuwa, muqawama na mapambano ya taifa la Palestina yanafanyika kwa ajili ya kujihami na kulinda matukufu ya taifa hilo.

Baada ya kutokea operesheni ya kishujaa ya mwanamapambano wa Palestina huko Tel Aviv ikiwa ni kujibu jinai za kila leo za Israel, ubalozi wa Uturuki katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni pamoja na wizara ya mambo ya nje ya Bahrain zimetoa taarifa ya kulaani operesheni hiyo ya mwanamuqawama wa Palestina.

Hazim Qasim pia ameashiria kuwa, nchi za Uturuki na Bahrain zinapaswa kulaani kwanza jinai zinazofanywa kila leo na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na amesema, wanajeshi wa Israel wanafanya jinai kubwa dhidi ya Wapalestina na matukufu yao na huo ni ugaidi wa wazi na ni ubaguzi usiokanushika na kwamba mapambano dhidi ya utawala wa kigaidi wa Israel ni haki inayotambuliwa kimataifa. 

342/