Katika ripoti yake, UNICEF imesema watoto wanakabiliwa na hatari ya magonjwa mbalimbali yanayotokana na maji machafu, tushio la kuzama na kuna hatari pia ya utapiamlo kuwakumba kutokana na mafuriko hayo katika taifa hilo la kusini mwa Asia.
Mafuriko hayo yaliyotokana na mvua kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miongo mitatu, yamesababisha vifo vya watu 1,200 tangu katikati ya mwezi Juni na zaidi ya watu milioni 33 wameathirika, wengi wao wakiwa kusini na kusini magharibi mwa nchi hiyo, maeneo ambayo ni maskini mno.
342/