Shirika la habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- linaripoti kuwa takwimu hizi zimekusanywa kwa kutumia mfumo wa kuhesabu kielektroniki unaotumia akili bandia (AI), ambao unarekodi idadi ya wahudhuriaji wanaoingia Karbala kupitia njia tano kuu:
1. Baghdad → Karbala
2. Baghdad → Al-Jamaliya
3. Najaf → Karbala
4. Babil → Karbala
5. Husayniya → Karbala.
Wakuu wa Haram wamesema kuwa mfumo huu umekuwa ukifanyakazi kwa mfululizo kwa miaka 10, na unakusanya data kwa wakati halisi.
Katika taarifa yao, Haram Tukufu ya Abasi iliongeza:
“Tunatoa rambirambi zetu kwa Imam wa Zama (a.j), marjaa wakuu, na ummah ya Kiislamu kwa heshima ya Arubaini ya Imam Hussein (a.s), na tunaomba Mwenyezi Mungu awarudishe mahujaji salama na kwa ajili ya ibada zao zilizokubalika.”
Your Comment