Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Naibu Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Ali Bagheri, amesema kuwa Marekani haiwezi kuaminika kutokana na kile alichokitaja kuwa ni tabia ya nchi hiyo ya kuvunja ahadi na makubaliano ya kimataifa.
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Mayadeen, Bagheri amesisitiza kuwa Iran inategemea uwezo wake wa ndani usiotangazwa, pamoja na vikosi vyake vya ulinzi na wananchi wake katika kukabiliana na kile alichokiita mashambulizi na vitisho.
Ameongeza kuwa chanzo kikuu cha ukosefu wa utulivu na usalama katika eneo la Mashariki ya Kati ni uwepo wa Marekani na Israel, akisisitiza kuwa mataifa hayo mawili yanaendelea kuchochea migogoro katika kanda hiyo.
Aidha, Bagheri ameeleza kuwa kukomesha vita katika nyanja zote, ikiwa ni pamoja na Lebanon, ni miongoni mwa misingi muhimu katika mazungumzo yoyote au makubaliano ya kisiasa yanayoweza kufikiwa.
Your Comment