Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya umejibu kwa ukosoaji mkali taarifa ya hivi karibuni ya Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM), iliyodai kuwa ilifanikiwa kuyazuia makombora yote ya Iran na kuliharibu kikamilifu jeshi la Iran.
Kupitia akaunti yake rasmi kwenye mtandao wa kijamii, ubalozi huo uliandika kwa kejeli: "Endeleeni kudanganya, marafiki. Kitu pekee kilichoharibiwa ni sifa yenu."
Ubalozi huo uliongeza kuwa, kinyume na madai ya Marekani, wakati wa operesheni za makombora za Iran, rada mbili muhimu za kijeshi za Marekani katika eneo hilo ziliharibiwa.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, rada zilizotajwa ni:
1_Rada ya ASR-1000 katika Kambi ya Anga ya Ali Al Salem nchini Kuwait, ambayo ilidaiwa kuharibiwa.
2_Rada ya TPS-59 nchini Bahrain, ambayo pia ilidaiwa kuharibiwa.
Ubalozi wa Iran ulisisitiza kuwa madai ya Marekani hayalingani na hali halisi ya matukio yaliyotokea uwanjani, ukidai kuwa taarifa hizo zinalenga kuficha hasara zilizopatikana wakati wa mashambulizi hayo.
Your Comment