23 Juni 2026 - 13:37
Rais Pezeshkian: Sera za Kivamizi za Utawala wa Kizayuni Ndizo Chanzo cha Ukosefu wa Usalama katika Eneo

Rais Masoud Pezeshkian amesema sera za uchokozi za utawala wa Kizayuni ndizo chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama katika eneo, huku Iran na Serbia zikisisitiza umuhimu wa kuimarisha amani, utulivu na ushirikiano wa pande mbili.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) - ABNA - Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, na Rais wa Serbia, Aleksandar Vučić, wamekaribisha makubaliano yaliyofikiwa ya kusitisha vita na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha amani na utulivu katika eneo, sambamba na kuendeleza ushirikiano wa pande mbili kati ya nchi zao.

Katika mazungumzo ya simu kati ya viongozi hao wawili, Rais Pezeshkian alitoa shukrani zake kwa serikali na wananchi wa Serbia kwa misimamo yao ya wazi kuhusiana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, pamoja na misaada ya kibinadamu waliyoitoa wakati wa kipindi cha vita.

Rais wa Iran alisisitiza kuwa sera za kivamizi na uchokozi za utawala wa Kizayuni ndizo sababu kuu za kuendelea kuwepo kwa hali ya kutokuwa na usalama na mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati, akitoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kidiplomasia ili kudumisha amani ya kudumu.

Kwa upande wake, Rais wa Serbia Aleksandar Vučić alitoa salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi kwa kiongozi wa Iran, na kuthibitisha kuwa Serbia itatuma mwakilishi rasmi kushiriki katika shughuli za mazishi yake.

Aidha, Vučić alieleza kuthamini kwake misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono umoja wa ardhi na mamlaka ya kitaifa ya Serbia, akisema kuwa nchi yake inaendelea kuthamini uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha