7 Julai 2026 - 16:16
Marasimu ya Kumuaga Shahidi Sayyid Ali Khamenei yakamilika Qom, Mazishi Yataendelea Katika Miji ya Najaf na Karbala

Marasimu ya kihistoria ya kumuaga Shahidi Ayatollah Shahidi Sayyid Ali Khamenei yamehitimishwa katika Mji mji Mtakatifu wa Qom, huku mwili wake ukitarajiwa kuwasili Najaf usiku wa Kuamkia Jumatano kabla ya kupelekwa Najaf na Karbala kwa ajili ya mazishi

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Marasimu ya kihistoria ya kumuaga Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Shahidi Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, yamehitimishwa katika mji mtakatifu wa Qom baada ya kuhudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali.

Marasimu ya Kumuaga Shahidi Sayyid Ali Khamenei yakamilika Qom, Mazishi Yataendelea Katika Miji ya Najaf na Karbala

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa, mwili wa marehemu pamoja na miili ya baadhi ya wanafamilia wake utawasili katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq usiku huu, kabla ya kuendelea na marasimu ya mazishi katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala siku inayofuata.

Marasimu hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya waumini na waombolezaji kutoka Iraq na mataifa mengine, huku yakionekana kuwa miongoni mwa matukio makubwa ya kihistoria katika ukanda huo.

Marasimu ya Kumuaga Shahidi Sayyid Ali Khamenei yakamilika Qom, Mazishi Yataendelea Katika Miji ya Najaf na Karbala

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha