9 Julai 2026 - 13:38
Kisa cha Kihistoria:Jinsi na Kwa Nini Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashimi Nejad Aliuawa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq /MEK

Kwa mujibu wa simulizi za kihistoria, kuuawa kwa Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashimi Nejad mnamo mwaka 1981 kulikuwa sehemu ya mfululizo wa mauaji yaliyotekelezwa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq (MEK), likiwa na lengo la kuwaondoa viongozi waliokuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– kuuawa kwa Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashemi Nejad, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu kabla na baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, kunahesabiwa kuwa sehemu ya mfululizo wa mauaji yaliyotekelezwa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq (MEK), linalojulikana pia kwa jina la Munafiqeen, katika mwaka 1981.

Kisa cha Kihistoria:Jinsi na Kwa Nini Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashimi Nejad Aliuawa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq /MEK

Kwa mujibu wa maelezo ya kihistoria, chuki ya kundi hilo dhidi ya Hashemi Nejad ilianza tangu kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu, walipokutana naye gerezani. Mnamo miaka ya 1975 na 1976 alianza harakati zake za kisiasa kwa uwazi na ujasiri mkubwa, jambo lililosababisha kutiwa mbaroni pamoja na Sayyid Abbas Vaez Tabasi.

Hashemi Nejad alifungwa gerezani kwa muda wa miaka miwili. Akiwa gerezani mwaka 1977 alipata fursa ya kuyafahamu kwa undani mafundisho na itikadi potofu za makundi kama Mujahideen-e Khalq. Wakati huohuo, wanachama wa kundi hilo walipata nafasi ya kuifahamu vizuri fikra, misingi na msimamo wa Hashemi Nejad kuhusu Uislamu na Mapinduzi.

Kwa mujibu wa simulizi hizo, chuki kubwa ya MEK dhidi yake ilitokana na ukweli kwamba akiwa gerezani aliweza kutambua kwa karibu upotovu wao wa kiitikadi, namna walivyoutafsiri Uislamu na mbinu zao za kisiasa. Baada ya kuachiwa huru, aliendelea kuwashauri kwa hekima, upole na mawaidha ili warejee katika njia sahihi, licha ya kutambua wazi upotovu wa fikra zao.

Historia inaeleza kuwa viongozi wa MEK walikuwa wakitambua vyema uwezo mkubwa wa Hashemi Nejad katika masuala ya dini, siasa na jamii, pamoja na mchango wake mkubwa katika kuendeleza na kuimarisha Mapinduzi ya Kiislamu. Kutokana na sababu hiyo walifanya uamuzi wa kumuondoa, kama walivyowaua viongozi wengine wengi waliokuwa na nafasi muhimu katika kuimarisha mfumo wa Mapinduzi. Mauaji ya Rais Mohammad Ali Rajai na Waziri Mkuu Mohammad Javad Bahonar pia yalikuwa sehemu ya mkakati huo.

Asubuhi ya tarehe 28 Septemba 1981, baada ya kumaliza kipindi cha muhadhara wa kujibu maswali katika jengo la Chama cha Jamhuri ya Kiislamu tawi la Mashhad, Hashemi Nejad alipokuwa akishuka ngazi, alikaribiwa na mmoja wa wanachama wa Mujahideen-e Khalq aliyejulikana kwa jina la Hadi Alavi Fitilehji, ambaye hapo awali alikuwa amejipenyeza ndani ya chama hicho lakini baadaye akafichuliwa na kufukuzwa.

Kisa cha Kihistoria:Jinsi na Kwa Nini Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashimi Nejad Aliuawa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq /MEK

Kwa mujibu wa taarifa hizo, gaidi huyo aliweka bomu la mkononi kwenye tumbo la Shahidi Hashemi Nejad na kulilipua, jambo lililosababisha kuuawa kwake papo hapo. Katika mlipuko huo, mkono mmoja wa mshambuliaji ulikatika, huku mlinzi wa chama aliyeitwa Mohsen Tavakkoli na mmoja wa washiriki wa kipindi cha maswali na majibu, Ata Zarif, wakijeruhiwa.

Amir Yaghmaei, aliyewahi kuwa msaidizi wa mkuu wa kitengo cha ujasusi cha Mujahideen-e Khalq, amenukuliwa akisema kuwa mpango wa mauaji hayo uliandaliwa na wanachama wawili wa kundi hilo walioitwa Jalal na Shahab. Mwanzoni walipanga kulipua ukumbi mzima wa muhadhara, lakini baada ya kubaini kuwa Hadi Alavi alikuwa ameshafichuliwa, walibadilisha mpango.

Kwa mujibu wa maelezo hayo, viongozi wa kundi hilo walidai kuwa wakati huo Sayyid Abbas Vaez Tabasi alikuwa Makkah, na Hashemi Nejad ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa Mashhad. Kwa mtazamo wao, kumuua Hashemi Nejad kungedhoofisha kwa kiasi kikubwa mfumo wa Mapinduzi katika mji huo.

Ndipo Hadi Alavi, ambaye alikuwa akifanya kazi katika duka la kuuza vitabu karibu na eneo la Haram Tukufu ya Imam Ridha (as), akapewa bomu la mkononi. Alielekezwa kwenda katika makao ya Chama cha Jamhuri ya Kiislamu kwa kisingizio cha kununua vitabu na mabango, kisha amshambulie Hashemi Nejad mara tu atakapomaliza muhadhara wake na kutoka nje ya ukumbi. Mpango huo ulitekelezwa na kusababisha kuuawa kwake akiwa ni mmoja wa viongozi mashuhuri na wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran.

Kisa cha Kihistoria:Jinsi na Kwa Nini Shahidi Hujjatul Islam Sayyid Abdul Karim Hashimi Nejad Aliuawa na Shirika la Kigaidi la Mujahideen-e Khalq /MEK

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha