10 Julai 2026 - 09:59
Araghchi Amjibu Trump: Iran Haiombi Mazungumzo ya Makubaliano, Marekani Ndio Inayoomba Mazungumzo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amekanusha kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba Iran inaomba kufikiwa kwa makubaliano, akisisitiza kuwa ni Washington ambayo imekuwa ikiomba mazungumzo mara kwa mara huku Tehran ikitaka suluhisho la kudumu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Abbas Araghchi, amekanusha vikali kauli ya Rais wa Marekani Donald Trump aliyedai kuwa Iran "inaomba kwa udi na uvumba kufikiwa kwa makubaliano."

Akijibu madai hayo, Araghchi alisema kuwa Iran haiombi makubaliano yoyote, bali ni utawala wa Marekani ambao umekuwa ukiwasilisha maombi ya kufanya mazungumzo mara kwa mara, alisema Araghchi.

Aidha, Waziri huyo alisisitiza kuwa kurudia madai yale yale mara kwa mara hakuwezi kubadilisha hali halisi iliyopo, akieleza kwamba msimamo wa Iran umejengwa juu ya kulinda maslahi ya taifa na kufikia suluhisho la kudumu kupitia heshima na usawa katika mazungumzo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha