Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Philiph Hammond, amesema Iran ina mengi ya kunufaika iwapo italegeza baadhi ya misimamo yake na kuafikiana kikamilifu na nchi zenye nguvu zaidi duniani kuhusu mpango wake wa kinyuklia, huku muda wa mwisho wa kufikiwa makubaliano kamili ukitarajiwa kuwa Jumatatu ijayo. Hammond amesema Iran itaweza kuzifikia mali zake zilizozuiwa, itakuwa na uhuru wa kufanya biashara ulimwenguni na itaboresha uhusiano wake na jumuiya ya kimataifa. Wanadiplomasia wa Uingereza, Ufaransa, Urusi, China, Marekani, Ujerumani, Umoja wa Ulaya na Iran wamekuwa wakifanya mazungumzo tangu Jumanne mjini Vienna, Austria. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, inasemekana anaondoka kutoka kwenye mazungumzo hayo hii leo kuelekea Paris kushauriana na wenzake wa Ulaya.
Yafaa kuzingatia kuwa: Jamhuri ya kiislamu ya Iran imekataa kujadili mambo yaliyo nje ya mpango wa nyuklia ambayo yameingizwa kwenye mazungumzo hayo kama mashart ya kufikia muafaka.