3 Desemba 2014 - 10:21
Jeshi la Iran lafanya mashambulizi dhidi ya Daesh

Makao makuu ya jeshi la Marekani Pentangon limethibitisha kwamba ndege za kivita za jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran limefanya mashambulizi dhidi ya magaidi wa Daesh.

Makao makuu ya jeshi la Marekani Pentangon limethibitisha kwamba ndege za kivita za jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran limefanya mashambulizi dhidi ya magaidi wa Daesh.

 Mzungumzaji wa makao makuu ya jeshi ya Marekani kamanda John Kirby amesema kuwa: Mashambulizi haya yaliyofanywa na jeshi la Iran hayahusiani na muungano wa majeshi yetu yanayofanya mashambulizi Iraq, na kwamba siasa yetu bado iko pale pale pamoja na kwamba Iran imekuwa ikituomba ishirikiane nasi lakini sisi hatutaki ushirikiano na jeshi la Iran katika kukabiliana na magaidi wa Deash.

Kwa upande wa pili makao makuu ya Jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran kupitia Brigedia General Masoud Jazairi imetoa tamko kuwa: Sikweli kwamba Jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya kiislamu ya Iran limeomba kushirikiana na Marekani katika kupambana na magaidi wa Daesh, na wala jeshi hilo halina nia wa mpango wa kushirikiana Marekani katika mashambulizi dhidi ya magidi hao na kwamba Jeshi hilo linatambua kuwa Marekani ndiye mdhamini wa magaidi hao na ndiye chanzo cha machafuko ya mashariki yakati.

Majeshi ya jamhuri ya kiislamu ya Iran yamekuwa yakisaidia serikali ya Iraq, Syria na Wakurd katika kupambana na magaidi wa Daesh.

Serikali ya Iran imekuwa kitoa msaada wa silaha, mafunzo na mbinu za kupambana na magaidi hao, ambapo mpaka sasa mafanikio makubwa yanayoonekana katika nchi hizo yanasadikiwa kutokana na msaada wa serikali ya Iran.

Yafaa kushiria kwamba uhusiano wa Marekani na Iran uliharibika tangu Iran kufanya mapinduzi mwaka 1979 nakutangaza dola la kiislamu .

 

Lebo