7 Desemba 2014 - 18:35
Waasi waua watu 12 congo

Raia wasiopungua 12 wameuliwa kwa kukatwakatwa kwa mapanga na mashoka na watu wanaosadikiwa kuwa ni waasi kwenye kijiji cha Ahili kilichopo kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Raia wasiopungua thelathini na wanne wameuliwa  kwa kukatwakatwa kwa  mapanga na  mashoka na  watu  wanaosadikiwa kuwa ni waasi  kwenye kijiji cha Ahili  kilichopo  kaskazini  mashariki  mwa  Jamhuri  ya Kidemokrasi ya Kongo.

 Afisa mmoja wa kijiji hicho amesema  kuwa mauaji  hayo  yalifanyika  hapo  jana katika mfululizo  wa mashambulio yanayoelekezwa kwa raia. Mkuu wa usimamizi   wa utawala  katika kijiji cha  jirani amesema  waasi walikilenga kijiji cha Ahili  kilichopo umbali  wa kilometa  10 kutoka  mji wa Oicha katika jimbo la Beni. Watu wanaotuhumiwa  kuwa waasi walianza kuwashambulia  wanakijiji saa moja  jioni wakati  wanakijiji walipokuwa kwenye  mashamba  yao na hivyo  ilikuwa  vigumu kwao kupiga mbiu  ya mgambo. Viongozi wa serikali  pamoja  na  asasi za kiraia zimelilaumu  kundi la ADF kwa mauaji hayo. Kundi  hilo  la  siri liliundwa  mnamo miaka  ya 90 kupambana na  serikali ya Uganda. Mpaka sasa  raia zaidi 250 wameshauawa tokea mwezi  wa Oktoba katika jimbo la Beni na maeneo jirani.

Yafaa kuashiria kuwa kutokana na utajiri na rasilimali za nchi ya Congo waatu wengi wamekuwa wakitamani mali za nchi hiyo na hivyo kusababisha uasi na uporaji wa mali na maeneo muhimu.

Lebo