-
Ayatollah Nouri Hamedani: Jumuiya za Kisayansi za Hawza, ni mahala salama kwa mawazo mapya na safi
Ayatollah Nouri Hamedani Marjii Taqlid wa Madhehebu ya Shia ametoa ujumbe wake katika Mkutano wa vyama (jumuiya) vya Kisayansi vya Seminari (Hawza) ya Qom.
-
Kwa nini Israel na Marekani zinaeneza chuki dhidi ya Uislamu kwa kutumia vibaya vyombo vya habari?
Utawala wa Kizayuni wa Israel na Marekani pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya zimeendeleza vitendo vyao vya uharibifu na kuiondoa Televisheni ya Al-Aqsa katika satalaiti zote za kimataifa kwa lengo la kubana uhuru wa kujieleza.
-
Rais wa China akataa mwaliko wa EU wa kuhudhuria kikao cha kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano
Rais Xi Jinping wa China amekataa mwaliko wa kuhudhuria kikao kilichopangwa kufanyika mjini Brussels kuadhimisha miaka 50 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya.
-
Hizbullah: Lebanon haitaanzisha katu uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni Israel
Mwakilishi wa Hizbullah katika Bunge la Lebanon amesisitizia msimamo wa kudumu wa nchi hiyo kuhusiana na utawala wa Kizayuni wa Israel na akasema, Lebanon kamwe haitokubali kufuata mkondo wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na utawala huo ghasibu.
-
UNICEF: Asilimia 90 ya wakazi wa Ghaza wanashindwa kupata maji safi ya kunywa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetahadharisha kuwa uhaba mkubwa wa maji katika Ukanda wa Ghaza umefikia hatua mbaya na ya maafa, kwa ababu karibu asilimia 90 ya wakazi wa eneo hilo wanashindwa kupata maji safi ya kunywa.
-
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vyaishambulia kwa mara ya pili manowari ya kubebea ndege za kivita ya US
Vikosi vya Ulinzi vya Yemen vimeishambulia kwa mara ya pili manowari ya kubebea ndege za kivita ya Marekani ya USS Harry Truman na kuzima mashambulizi ya anga yaliyokuwa yamedhamiriwa kufanywa na Washington dhidi ya nchi hiyo.
-
Hamas: Vitisho vya Marekani vinatatiza zaidi hali ya mambo
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesisitiza kuwa: Vitisho vya Marekani vinapelekea tu hali ya mambo kuwa ngumu zaidi.
-
Israel imeficha gharama za vita
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kuwa gharama za vita za utawala huo zimefichwa mwaka huu, tofauti na ripoti za mwaka jana, na kuna wasiwasi kuhusu usimamizi wa bajeti.
-
Baqaei: Chanzo cha ukosefu wa amani Asia Magharibi ni mauaji na kukaliwa Palestina
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hujuma za majeshi ya Marekani na Uingereza dhidi ya Yemen na kusema kuwa, mzizi wa ukosefu wa usalama katika eneo la Magharibi mwa Asia ni kuendelea mauaji na kukaliwa kwa mabavu ardhi ya Palestina.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu: Bila shaka yoyote taifa la Yemen litaibuka mshindi
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amelipongeza taifa la Yemen kwa Muqawama wake wa kukabiliana na jinai za kinyama za utawala wa Marekani dhidi ya nchi hiyo na kusisitiza kuwa hakuna shaka yoyote taifa la Yemen litaibuka mshindi.
-
Sisitizo la Iran la kukabiliana na siasa za mabavu za Marekani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi alisema Jumapili, Machi 16, katika kujibu matamshi ya kibabe na ya uingiliaji ya viongozi wa Marekani dhidi ya Iran, kwamba serikali ya Washington haina haki ya kuilazimisha Iran itekeleze siasa za kigeni zinazoendana na maslahi ya Washington.
-
Baqaei: Jumbe za Marekani zinakinzana
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa jumbe zinazotoka Marekani zinakinzana yaani sambamba na kubainisha kuwa nchi hiyo iko tayari kufanya mazungumzo, wakati huo huo vikwazo vikubwa vinawekwa kwa sekta mbalimbali za kibiashara na uzalishaji za Iran.
-
Mauaji ya raia 2 wa Lebanon kupitia magaidi wa Al-Julani
Magaidi wa Al-Julani wamefanya jinai nyingine katika maeneo ya mpakani mwa Lebanon na Syria.
-
Video | Sherehe ya kufunga warsha ya "Wanawake na Upinzani (Muqawamah)" iliyoandaliwa na Tamasha la Kimataifa la Filamu la Upinzani (Muqawamah).
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Hafla ya kufunga warsha ya "Wanawake na Upinzani (Muqawamah)" iliyoandaliwa na Tamasha la Kimataifa la Filamu la Upinzani (Muqawamah) sambamba na uwepo wa watengenezaji Filamu wa Kimataifa kutoka Urusi, Azerbaijan, Afghanistan, Pakistan, India, Kashmir, Venezuela, Lebanon, Syria, Iraq, Tajikistan, Bangladesh, Saudi Arabia, Palestina, Yemen, Uingereza, Indonesia, China, Myanmar, Uturuki na Nigeria, ikiambatana na Hotuba ya Katibu wa Tamasha hili, imefanyika katika Kitivo cha Sanaa na Vyombo vya Habari cha Shahid Avini.
-
Ripoti ya Picha | Kusherehekea Saumu ya Kwanza katika Zainabiyah, Isfahan
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Sherehe ya mfungo wa kwanza imefanyika katika madhabahu takatifu ya Isfahan ya Zainabiyah (s.a) kwa mahudhurio makubwa ya shauku ya vijana.
-
Video | Uwekaji wa Meza ya Iftar katika Mji wa mpakani Kusini mwa Lebanon
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (A.S) - Abna – Meza ya chakula cha Iftar kwa wafungaji wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, iliwekwa katika Uwanja Mkuu wa mpaka wa Mji wa "Al-Khayyam" Kusini mwa Lebanon. Wakati wa vita vya hivi karibuni, Mji huu ulikuwa mlengwa wa mashambulizi makali zaidi ya anga na ardhini ya jeshi haram la Kizayuni.
-
Katika kukabiliana na mashambulizi ya Marekani... Yemen inakabiliana na ongezeko la mvutano kwa ongezeko la mvutano
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -: Vikosi vya jeshi la Yemen vimelenga (vimeishambulia) Meli ya kubebea ndege za Kivita ya USS Truman katika Bahari Nyekundu kwa mara ya pili ndani ya masaa 24 kwa kutumia Makombora ya Balistiki na Mbawa na Droni (Ndege za mashambulkizi zisizokuwa na rubani). Kiongozi wa vuguvugu la Ansarullah la Yemen, Sayyid Abdul Malik Al-Houthi, amethibitisha kuwa Yemen itakabiliana na hali yoyote ya ongezeko la kasi ya mvutano kwa ongezeko la kasi ya mvutano.
-
Radiamali ya Seneta RajA Nasser kwa mauaji ya Mwanazuoni wa Pakistan
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amelaani mauaji ya Mufti Munir Shakir, Mwanazuoni wa Kisunni wa Pakistan, na kuyataja kuwa ni hasara isiyoweza kufidiwa.
-
Dk. Pezeshkian: Ikiwa mwongozo wa Qur'an hauonekani katika matendo na maisha yetu, basi tunapaswa kufikiria upya tabia zetu.
Akisisitiza umuhimu wa kuunganisha maarifa ya Qur'an na matendo ya kijamii, Rais wa Iran amesema: Tatizo kubwa ni pengo kati ya kuijua na kuitekeleza Qur'an. Tunadai kuwa Qur’an inatuonyesha njia ya uongofu na inamfikisha Mwanadamu katika kilele cha juu zaidi, lakini ikiwa kivitendo hakuna dalili ya mwongozo huu inayoweza kuonekana katika maisha yetu ya kibinafsi na ya kijamii, basi kwa hakika tunapaswa kuangalia upya tabia zetu.
-
Sayyid Abdul Malik al-Houthi: Meli za Marekani ni marufuku pia kupita Bahari Nyekundu
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema: Tutajibu ongezeko la mvutano kwa ongezeko la mvutano. Kuanzia sasa, sambamba na kupiga marufuku kupita kwa meli za Israeli katika Bahari Nyekundu, kupita kwa meli za Marekani pia ni marufuku.