22 Mei 2025 - 00:00
Ansarullah: Operesheni za Kijeshi za Yemen Zitaendelea Kuongezeka Taratibu

Mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah Yemen amesisitiza kuwa ikiwa uvamizi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza utaendelea, basi operesheni za kijeshi za Yemen zitaendelea kuongezeka taratibu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Ansarullah: Tumefanikiwa Kufunga Bandari ya Eilat na Kuweka Uzingirizi wa Anga Kwenye Uwanja wa Ndege wa Ben GurionMuhammad al-Bukhaiti, mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Ansarullah ya Yemen, katika mahojiano na televisheni ya Al Jazeera, amesema:

“Hadi sasa tumefanikiwa kuufunga bandari ya Eilat na kuweka uwanja wa ndege wa Ben Gurion katika hali ya kuzingirwa kwa njia ya anga.”

Akaongeza:

“Tunazo chaguzi nyingi na mbalimbali za kuendeleza na kuongeza mashinikizo ya kijeshi dhidi ya wavamizi wa Kizayuni.”

Al-Bukhaiti pia alisisitiza kuwa moja ya malengo ya operesheni za msaada za Ansarullah kwa Ukanda wa Gaza ni

Kuimarisha msimamo wa Harakati ya Hamas katika mazungumzo dhidi ya wavamizi.

Vilevile alieleza:

Tuna utayari kamili kukabiliana na aina yoyote ya mashambulizi ya kijeshi kutoka kwa utawala wa Kizayuni.

Aidha, jeshi la Yemen lilikuwa tayari limetangaza kupitia taarifa rasmi kuwa:

“Kwa mujibu wa amri ya uongozi wetu na kwa kutegemea msaada wa Mwenyezi Mungu, tumeanza kutekeleza mpango wa kuzingira baharini Bandari ya Haifa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha