Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limekanusha taarifa zilizosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari zikidai kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon, Sheikh Naim Qassem, ameuawa katika shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel lililolenga eneo la Dahiyeh, kusini mwa mji wa Beirut, siku ya Jumapili.
Katika taarifa yake, IRGC ilieleza kuwa madai hayo hayana ukweli wowote na ni sehemu ya vita vya kisaikolojia vinavyolenga kueneza taarifa za upotoshaji na kuvuruga hali ya kambi ya Muqawama.
Jeshi hilo limesisitiza kuwa taarifa rasmi pekee ndizo zinazopaswa kuaminiwa kuhusu maendeleo yanayohusu viongozi wa Muqawama, huku likitoa wito kwa wananchi kutopuuzia au kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa.
Your Comment