IRGC
-
IRGC Yalenga Kambi ya Camp Titin Jordan, Yathibitisha Kuharibu Kabisa Miundombinu Muhimu ya Jeshi la Marekani
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limetangaza kutekeleza shambulizi la makombora ya balistiki dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani ya Camp Titin nchini Jordan, likisema hatua hiyo ni sehemu ya operesheni ya kulipiza kisasi dhidi ya kile lilichokiita uchokozi wa Marekani.
-
IRGC yashambulia kwa makombora kambi ya Marekani ya Prince Hassan nchini Jordan
IRGC imesema imetekeleza shambulio zito la makombora ya balestiki dhidi ya vituo vya ndege zisizo na rubani za masafa marefu aina ya RQ-4 na MQ-9 katika kambi ya anga ya Marekani ya Prince Hassan nchini Jordan. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shambulio hilo lilifanywa kulipiza kisasi baada ya shambulio la Marekani katika hafla ya ndoa huko Sirik, Hormozgan, Iran. IRGC inadai kuwa baadhi ya ndege zisizo na rubani ziliharibiwa, huku baadhi ya marubani na mafundi wa ndege hizo wakiuawa, na miundombinu kadhaa ya kiufundi kuchomwa moto.
-
Mashambulizi ya Jeshi la Kigaidi la Marekani dhidi ya Maeneo ya Kusini mwa Nchi ya Iran
CENTCOM imetangaza: Vikosi vya Marekani leo saa 12:00 mchana kwa saa za Mashariki mwa Marekani vilianza mashambulizi dhidi ya malengo ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Iran.
-
IRGC: Udhibiti wa Iran Juu ya Mlango wa Hormuz ni Kamili na wa Uamuzi
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limesema lina udhibiti kamili na madhubuti juu ya Mlango wa Hormuz, likikanusha madai ya Marekani kwamba njia hiyo iko wazi kwa usafiri wa kimataifa.
-
IRGC: Hatutaruhusu adui kufanya harakati za ardhini nchini Iran
Kamanda wa Kambi ya Hamza Sayyid al-Shuhada ya Kikosi cha Ardhini cha IRGC amesema adui alijaribu kutumia vita vya tatu vilivyolazimishwa kuleta mpasuko miongoni mwa wananchi, kuchochea ukosefu wa usalama na kulenga mshikamano wa kijamii, lakini vikosi vya Iran havikuruhusu kupenya wala harakati za ardhini za adui.
-
Mkuu wa Walinzi wa Mapinduzi: Ushiriki Endelevu wa Wananchi Ni Muhimu kwa Kuimarisha Umoja na Muqawama
Brigedia Jenerali Hossein Maroufi amesema kuendelea kwa ushiriki madhubuti wa wananchi katika nyanja mbalimbali ni muhimu kwa kuimarisha umoja wa kitaifa na kuunga mkono Muqawama.
-
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Nchi zinazosaidia mchokozi zitapokea jibu kali
IRGC imetahadharisha kuwa nchi zinazosaidia Marekani zinaweza kukabiliwa na jibu kali iwapo hazitabadilisha mwenendo wao. Pia imesema vikosi vya majini vya Iran vina udhibiti wa Mlango wa Hormuz, ambao Iran inasema utaendelea kufungwa huku vitisho na uingiliaji wa Marekani katika eneo hilo vikiendelea. IRGC imeonya kuwa hatua hizo zinaweza kuongeza zaidi mvutano na kuzidisha hali ya usalama katika eneo.
-
IRGC: Ndege tatu za F-35 za Marekani zaangamizwa, nyingine tatu ziharibiwa katika kituo cha Al-Azraq nchini Jordan
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limefanya shambulizi la makombora dhidi ya Kituo cha Anga cha Al-Azraq nchini Jordan, likidai kuangamiza ndege tatu za kivita aina ya F-35 na kuharibu vibaya nyingine tatu, katika kile ilichokitaja kuwa ni kulipiza kisasi dhidi ya mashambulizi ya Marekani yaliyolenga nyumba za raia katika Kisiwa cha Qeshm.
-
IRGC Yatangaza Kumuua Mshukiwa wa Kundi la Kigaidi katika Mji wa Bukan
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kumuua mtu aliyemtaja kuwa mshukiwa wa ugaidi katika mji wa Bukan, mkoani Azerbaijan Magharibi, likisema alikuwa akijiandaa kutekeleza mashambulizi ya mauaji na vitendo vinavyohatarisha usalama.
-
IRGC: Iran Haina Chaguo Zaidi ya Kujibu Mashambulizi ya Marekani kwa Mujibu wa Qur’an
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limesema kuwa, kutokana na kutokuwepo kwa taasisi ya kimataifa yenye uwezo au utayari wa kuzuia mashambulizi ya Marekani dhidi ya hospitali, madaraja, reli, viwanja vya ndege, bandari, vituo vya mawasiliano na miundombinu mingine ya kiraia, Iran inalazimika kujibu kwa mujibu wa amri ya Qur’ani: “Na wakikushambulieni, nanyi washambulieni kwa mfano wa yale waliyokushambulieni.”
-
IRGC Yathibitisha kuharibu rada za Marekani za udhibiti wa baharini na anga nchini Oman
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuharibu rada za Marekani za udhibiti wa baharini katika Miamba ya Salamah na rada ya udhibiti wa anga katika eneo la Ghanam nchini Oman, katika mwendelezo wa operesheni iliyopewa jina la "Nasr 2 / Ushindi 2".
-
IRGC Yatangaza Kuiangusha Ndege ya Marekani Isiyo na Rubani Aina ya MQ-9 Kusini mwa Iran
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limetangaza kuwa limeiangusha ndege ya Marekani isiyo na rubani aina ya MQ-9 katika anga ya mji wa Khormuj, mkoani Bushehr, kufuatia kile ilichokitaja kuwa mashambulizi ya anga ya Marekani.
-
Mshauri wa Kamanda wa IRGC: Mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Yatakuwa Chachu ya Mabadiliko Makubwa Kanda ya Mashariki ya Kati
Mshauri wa Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kuwa mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, yatakuwa hatua muhimu itakayochochea maendeleo na mabadiliko ya kisiasa katika eneo la Mashariki ya Kati.
-
IRGC Yakanusha Taarifa za Kuuawa kwa Katibu Mkuu wa Hizbullah Sheikh Naim Qassem
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) limezitaja kuwa za uongo taarifa zinazodai kuwa Katibu Mkuu wa Hizbullah, Sheikh Naim Qassem, ameuawa katika shambulio la Israel kusini mwa Beirut, likisema ni sehemu ya vita vya kisaikolojia na upotoshaji wa habari.
-
IRGC: Vikosi vya Iran Viko Tayari Kujibu Uchokozi Wowote kwa Nguvu
Naibu Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Brigedia Jenerali Yadollah Javani, amesema silaha yenye nguvu zaidi ya Iran ni imani na itikadi ya wananchi wake, akisisitiza kuwa diplomasia na uwezo wa kijeshi vinaenda sambamba katika kulinda haki na maslahi ya taifa.
-
IRGC Yathibitisha Kushambulia Makao Makuu ya Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani Bahrain Kwa Kutumia Droni
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) wamedai kufanya shambulizi la ndege zisizo na rubani dhidi ya makao makuu ya Kikosi cha Tano cha Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Bahrain, katika kile walichokiita kujibu mashambulizi dhidi ya maeneo ya kusini mwa Iran.
-
IRGC Yadai Kuilenga na Kuiangusha Ndege Ndege Isiyo na Rubani ya Marekani MQ-9 Nchini Bushehr
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) wametangaza kuuangusha ndege isiyo na rubani ya kijeshi ya Marekani aina ya MQ-9 katika Mkoa wa Bushehr kusini mwa Iran.
-
IRGC Yadai Kushambulia Malengo Manne ya Kijeshi ya Marekani Nchini Jordan
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) wamedai kufanya mashambulizi ya makombora yaliyolenga maeneo manne muhimu ya kijeshi ya Marekani katika kambi ya Al-Azraq nchini Jordan, ikiwa ni pamoja na kituo cha amri na udhibiti.
-
Iran Yadai Meli za Marekani Zimeondoka Bahari ya Oman Baada ya Onyo la Kijeshi
Jeshi la Majini la Iran limetangaza kuwa meli za kivita za Marekani, USS Truxtun na USS Mason, zimeondoka Bahari ya Oman kuelekea Bahari ya Hindi kufuatia kile Iran inachokiita hatua za onyo za kijeshi zilizochukuliwa dhidi yao.
-
Iran Yadungua Ndege ya Marekani Isiyo na Rubani Baada ya Kukiuka Anga ya Nchi Hiyo
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeripotiwa kudungua ndege ya Marekani isiyo na rubani aina ya MQ-1 Predator baada ya kuingia katika anga ya Iran, tukio lililotajwa kuwa ukiukaji wa makubaliano ya usitishaji mapigano.
-
IRGC Yatangaza Mashambulizi ya Kulipiza Kisasi Dhidi ya Kambi ya Marekani
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limesema limelenga kambi ya kijeshi ya Marekani baada ya shambulizi lililoripotiwa kufanywa karibu na Uwanja wa Ndege wa Bandar Abbas, likionya kuwa uchokozi wowote dhidi ya Iran utakabiliwa na majibu makali zaidi.
-
IRGC: Ndege za Marekani za RQ-4 na F-35 Zalikimbia Baada ya Kujibiwa na Ulinzi wa Anga wa Iran
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kudungua ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 na kulazimisha ndege ya RQ-4 pamoja na ndege ya kivita ya F-35 kuondoka katika anga ya Iran baada ya kujibiwa na mifumo ya ulinzi wa anga. IRGC imeonya kuwa uvunjaji wowote wa usitishaji mapigano utakabiliwa na majibu makali ya kulipiza kisasi.