Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (Islamic Revolutionary Guard Corps) wametangaza alfajiri ya Jumatano kuwa wameikamata na kuiangusha ndege isiyo na rubani ya kijeshi ya Marekani aina ya MQ-9 katika Mkoa wa Bushehr.
Taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma ya IRGC imesema kuwa tukio hilo limetokea wakati wa mapigano ya anga yanayoendelea katika eneo la Mlango wa Hormuz, ambapo ndege hiyo isiyo na rubani ilijaribu kuingia na kuingilia eneo la mapigano kutoka upande wa kaskazini wa Ghuba ya Uajemi.
IRGC imeeleza kuwa ndege hiyo ililengwa na Silaha ya moto ya mifumo ya kisasa ya ulinzi wa anga ya Walinzi wa Mapinduzi katika anga ya mji wa Jam, Mkoa wa Bushehr, na hatimaye kuharibiwa.
Jeshi hilo limeongeza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya majibu yake dhidi ya kile kinachotajwa kuwa ni uvunjaji wa anga na uchokozi unaoendelea katika eneo hilo, likisisitiza kuwa litaendelea kulinda anga ya Iran dhidi ya vitisho vyovyote vya nje.
10 Juni 2026 - 13:03
News ID: 1825347
Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) wametangaza kuuangusha ndege isiyo na rubani ya kijeshi ya Marekani aina ya MQ-9 katika Mkoa wa Bushehr kusini mwa Iran.
Your Comment