Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC), Brigedia Jenerali Hussein Mohebi, ametangaza kuwa vikosi vya ulinzi wa anga vya IRGC vimeiangusha ndege ya Marekani isiyo na rubani aina ya MQ-9 katika anga ya mji wa Khormuj, mkoani Bushehr, kusini mwa Iran.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tukio hilo lilitokea baada ya kile IRGC ilichokieleza kuwa mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la Marekani alfajiri ya leo dhidi ya maeneo ndani ya Iran.
Brigedia Jenerali Mohebi amesema kuwa ndege hiyo ya MQ-9 ililengwa na kushambuliwa na mfumo wa ulinzi wa anga wa IRGC mara ilipoingia katika eneo husika, na kuangushwa kwa mafanikio.
Your Comment