8 Julai 2026 - 10:40
Rais wa Iran Masoud Pezeshkian Awasili Najaf Kushiriki Mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Masoud Pezeshkian, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf nchini Iraq kwa ajili ya kushiriki katika mazishi ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ambapo alipokelewa na Waziri Mkuu wa Iraq pamoja na viongozi wengine waandamizi wa nchi hiyo.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Masoud Pezeshkian, amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf nchini Iraq kwa ajili ya kushiriki katika shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei (Quddisa Sirruh).

Dkt. Pezeshkian alipokelewa katika uwanja huo wa ndege na Waziri Mkuu wa Iraq pamoja na kundi la viongozi waandamizi wa serikali ya Iraq, kabla ya kuelekea kushiriki katika shughuli za maombolezo na mazishi zitakazofanyika katika mji mtakatifu wa Najaf.

Kushiriki kwa Rais wa Iran katika shughuli hizo kunadhihirisha umuhimu wa tukio hilo, ambalo limewakutanisha viongozi wa kisiasa, kidini na maelfu ya waombolezaji kutoka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Kiongozi huyo Shahidi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha