17 Julai 2026 - 15:10
IRGC Yathibitisha kuharibu rada za Marekani za udhibiti wa baharini na anga nchini Oman

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limedai kuharibu rada za Marekani za udhibiti wa baharini katika Miamba ya Salamah na rada ya udhibiti wa anga katika eneo la Ghanam nchini Oman, katika mwendelezo wa operesheni iliyopewa jina la "Nasr 2 / Ushindi 2".

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza katika taarifa yake ya ishirini na moja kuhusu operesheni ya Nasr 2 kuwa vikosi vyake vya majini vimefanya mashambulizi yaliyolenga rada za Marekani nchini Oman.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashambulizi hayo yalifanyika alfajiri katika wimbi la kumi na tatu la operesheni Nasr 2, kwa kaulimbiu "Ya Aba Abdillah Al-Husayn (as)", ambapo IRGC ilidai kuharibu rada ya udhibiti wa baharini iliyoko katika Miamba ya Salamah pamoja na rada ya udhibiti wa anga ya Marekani iliyokuwa katika eneo la Ghanam nchini Oman.
 
IRGC imeeleza kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya hatua zake za kujibu mashambulizi dhidi ya Iran, ikisisitiza kuwa operesheni za kulipiza kisasi zitaendelea kwa uthabiti.
 
Aidha, katika taarifa hiyo, IRGC imesema kuwa Mlango wa Hormuz unaendelea kuwa chini ya usimamizi na uwezo wa vikosi vyake vya majini.
 

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha