15 Juni 2026 - 10:23
Mehr Yafichua Rasimu ya Makubaliano ya Vipengele 14 Kati ya Iran na Marekani

Shirika la Habari la Mehr limechapisha maelezo ya rasimu ya makubaliano yenye vipengele 14 kati ya Iran na Marekani, ikijumuisha kusitishwa kwa vita, kuondolewa kwa vikwazo, kufunguliwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, kurejeshwa kwa fedha za Iran na mazungumzo kuhusu nyuklia, huku ikisisitiza kuwa mpango wa makombora wa Iran na uhusiano wake na Muqawama havitakuwa sehemu ya makubaliano hayo.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA–, Shirika la Habari la Mehr limechapisha maelezo ya rasimu ya makubaliano yenye vipengele 14 vinavyodaiwa kufikiwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani, yakilenga kumaliza mvutano kati ya pande hizo na kuweka msingi wa mazungumzo ya mwisho kuhusu masuala ya nyuklia, kuondolewa kwa vikwazo na ushirikiano wa kiuchumi.

Kwa mujibu wa Mehr, rasimu hiyo inajumuisha vipengele vifuatavyo:
1. Kusitishwa mara moja na kwa kudumu kwa vita katika nyanja zote, ikiwemo nchini Lebanon.
2. Marekani kujitolea kutokuingilia masuala ya ndani ya Iran na kuheshimu uhuru na mamlaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
3. Kuondolewa kabisa kwa mzingiro wa baharini dhidi ya Iran ndani ya siku 30.

4. Marekani kujitolea kuondoa majeshi yake yaliyoko karibu na Iran.
5. Kufunguliwa tena kwa Mlango-Bahari wa Hormuz ndani ya siku 30 kwa mpango wa Iran.
6. Kusitishwa kwa vikwazo dhidi ya uuzaji wa mafuta na bidhaa za petrokemikali za Iran, pamoja na kurejeshwa kwa Iran haki ya kutumia kikamilifu rasilimali zake za kifedha.

7. Marekani na washirika wake kuwasilisha mpango wa ujenzi upya wa uchumi wa Iran wenye thamani ya angalau dola za Marekani bilioni 300.
8. Kufanyika kwa mazungumzo ya siku 60 ili kufikia makubaliano ya mwisho kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani na vya kimataifa.
9. Iran kuthibitisha tena chini ya Mkataba wa Kutokomeza Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) kwamba haitatengeneza silaha za nyuklia.

10. Marekani kutoweka majeshi mapya wala kuanzisha vikwazo vipya wakati mazungumzo yatakapokuwa yanaendelea.
11. Kuachiwa dola bilioni 24 za fedha za Iran zilizokuwa zimezuiwa, ambapo nusu ya fedha hizo itatolewa kabla ya kuanza kwa mazungumzo.
12. Kuundwa kwa mfumo maalumu wa kufuatilia utekelezaji wa makubaliano.

13. Makubaliano ya mwisho kupitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

14. Mazungumzo ya mwisho hayataanza kabla ya kutolewa kwa nusu ya fedha za Iran zilizozuiwa, kuondolewa kwa vikwazo vya mafuta na kuondolewa kwa mzingiro wa baharini. Aidha, rasimu hiyo inasisitiza kuwa makubaliano hayatagusa mpango wa makombora wa Iran wala uhusiano wake na makundi ya Muqawama, bali yatajikita katika masuala ya nyuklia, kuondolewa kwa vikwazo na ujenzi wa uchumi wa Iran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha